WAHITIMU 'CBE' WASHAURIWA KUWA WABUNIFU



Na Hellen Mtereko
MWANZA.




Kutokana na uhaba wa ajira nchini, wahitimu wa CBE campas ya Mwanza wameshariwa kuwa na maadili mema pamoja na kuendelea kuwa wabunifu ili kufikia malengo yao.

Akizungumza na wahitimu katika mahafali ya 14 ya chuo cha elimu ya biashara {CBE}kampasi ya Mwanza na mahafali ya 56 ya chuo hicho nchini, katibu mkuu wa wizara ya viwanda na biashara DKT. Dotto James  amesema, Kazi zipo isipokuwa wewe umejipangaje kuzifanya hizo kazi huwenda ni za kuajiriwa, kujiajiri, au kuajiri wenzako. 

''Taasisi za Fedha zipo na wanapesa za kukopesha isipokuwa mjipange, muandike andiko lenu vizuri, hizi benki zikishakuelewa haziwezi kukunyima pesa, tuwe wazalendo, heshima na maadili mema, tujitume ili tufikie malengo katika kulijenga taifa letu na kuondokana na watu ambao ni tegemezi''

''kuna kufanikiwa na kutokufanikiwa, kikubwa usikate tamaa, tuvae uzalendo wenye heshima, tupendane, ndiomtutakuwa na taifa lenye maendeleo'' Dkt. James 

Aidha Dkt. James ameupongeza uongozi wa Chuo hicho kwa kufanya vizuri na kuendelea kutoa elimu zaidi na mpaka sasa kinauwezo wa kudahili wanafunzi 2000 kutoka wanafunzi 400, hivyo serikali itaendelea kukitizama zaidi ili kuweza kumaliza changamoto ambazo wamezibainisha, kikubwa tunataka kiendelee kutoa wanafunzi wengi ili vijana wetu wapate elimu kama sera ya serikali inavyotaka.

Mkuu wa chuo cha elimu ya biashara {CBE}  Prof. Emmanuel Mjema amesema kuwa hatua wanazozichukua ili kuwaongezea uwezo wahitimu ni kuongeza mipango ambayo itawasaidia wanafunzi kuanzisha biashara zao zitakazosaidia kujiajiri, amesema wameanzisha pia mpango mwingine ambao mwanafunzi anakuwa anasoma huku anaendelea na masomo yake, ''Tumeona wanafunzi wengi hawana ujuzi wa kufanya biashara kwahiyo kupitia mikakati hii tutawasaidia wanafunzi wetu kujiajiri zaidi na kuajiri wengine, kikubwa waweze kunufaika na elimu wanayoipata hapa chuoni''




Prof. Mjema ameongeza kuwa, chuo cha CBE kinajitahidi kutoa wanafunzi wenye weledi mzuri kwahiyo anazidi kuishukuru serikalikwa kuwanunulia eneo hilo la chuo pamoja na majengo hivyo wataendelea kufanya vizuri zaidi, chuo cha CBE kimetoa watu wakubwa sana wakiwemo mawaziri, wafanyabiashara wakubwa kwahiyo hakuna kitakachorudisha nyuma na kushindwa kuwasaidia na kuwapa ujuzi vijana wetu  wenye ndoto kubwa ili kuinua nchi yetu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya uongozi wachuo cha elimu ya biashara Prof. Wineasta Anderson amesema lengo kubwa la chuo ni kutoa wahitimu wanaojitambua katika tasnia mbalimbali ikiwemo ujasiliamali ili kutengeneza Taifa la watu wanaojitegemea ili mwanafunzi akimaliza masomo yake akaajiri watu wengine.

Amesema, wahitimu wamepikwa vizuri hivyo wataenda kuwa mabalozi wazuri ili wasiende kuwa tegemezi, lakini chuo kina changamoto ambazo ameomba serikali iweze kuwatatulia zikiwemo za miundombinu ya barabara, umeme, na bweni la wanafunzi linahiotaji kufanyiwa ukarabati.




Jumla ya wahitimu 484 wametunukiwa Astashahada, Stashahada na Shahada, wanaume 257 sawa na asilimia 53 na wanawake 227 sawa na asilimia 47.  
 

Post a Comment

Previous Post Next Post