Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu, sera, uratibu, bunge, kazi, vijana, ajira, na wenye ulemavu Mhe. Jenister Mhagama, ametembelea maonyesho ya 21 ya africa mashariki ya wajasiliamali wadogo na wakati, yaliyohudhuliwa na nchi za afrika mashariki ambazo ni Rwanda, kenya, Uganda, Burundi, Sudani ya kusini na wenyeji Tanzania.
maonyesho haya yanafanyika mkoani mwanza kuanzia tarehe 2 mpaka tarehe 12 mwezi wa 12 ndani ya soko la afrika mashariki {rock city mall}
waziri Mhagama amesema mabanda ya wafanyabiashara wa tanzania ameona bidhaa zao kuwa na ubora kulingana na soko la afrika mashariki kukua kwa kiwango kikubwa na wajasiliamali wote wanapaswa kutumia fursa hii kama chachu ya kukua kiuchumi,
Jenister Mhagama ameongeza kuwa muunganiko huu wa nchi za afrika mashariki ni chanzo cha kukuza uchumi wa nchi na mfanyabiashara mmoja mmoja kutokana na mahusiano yatakayojengwa na muingiliano huu wa kibishara kutoka katika nchi sita za Afrika Mashariki
Post a Comment