AJALI YA TRENI TANGA..MTOTO MMOJA AFARIKI, WATANO WAJERUHIWA



Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 7 amefariki dunia baada ya Treni ya abiria yenye injini namba 9022 kupata ajali Wilayani  Pangani mkoani Tanga .

Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Reli Tanzania Jamila Mbarouk amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Januari 16, 2022 majira ya saa 10 Alfajiri kati ya Mkalamo na Mvave wilaya ya Pangani mkoani Tanga.

Jamila Amesema kuwa Treni hiyo iliondoka Arusha majira ya saa nane mchana siku ya Jumamosi kuelekea Dar es Salaam ikiwa na behewa 14 zilizobeba abiria 700 baada ya kufika eneo lililopo kati ya Mkalamo na Mvave  behewa 5 zilipinduka na nyingine 4 kuacha njia na kusababishakifo cha mtoto mmoja Hassan Lugano mwenye umri wa miaka 7 kufariki pamoja na abiria watano kujeruhiwa wakiwemo  Wanaume ni 3 na Wanawake 2.

Amesema kuwa Majeruhi tayari wamekimbizwa katika Zahanati ya Mkalamo kwa ajili ya kupatiwa matibabu na wanaendelea vizuri na kuongeza kiwa  Shirika hilo linaendelea kufuatilia kwa karibu kufahamu chanzo cha ajali ili kuchukua hatua.

Aidha Shirika la Reli Tanzania linatoa pole kwa familia ya marehemu na linawaombea majeruhi wa ajali wapate nafuu mapema ili waweze kuendelea na majukumu ya kujenga Taifa.

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post