ASKARI ANAYEDAIWA KUKAMATWA NA RUSHWA.. JESHI LA POLISI LATOA TAARIFA..HATUA KALI KUCHUKULIWA


Jeshi la Polisi limesema limeanza kuchukua hatua za kiuchunguzi kwa kushirikiana na wadau wengine kufuatia kusambaa mitandaoni kwa picha askari wa usalama barabarani mitandaoni zikimuonesha akiwa ameshika fedha zinazodaiwa kuwa ni za rushwa.


Taarifa iliyotolewa leo January 20,2022 na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini SACP David A. Misime imeeleza 
 kuwa hakuna aliyepo juu ya sheria, hivyo hatua kali na stahiki zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu mara ushahidi utakapopatikana.

"Hakuna aliyepo juu ya sheria hivyo hatua kali na stahiki kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu na ushahidi utakaopatikana zitachukuliwa." - Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David A. Misime



Post a Comment

Previous Post Next Post