m
Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Roselyn Nafuna mwenye umri wa miaka 39 amefariki baada ya kushambuliwa na mbwa wa mwajiri wake, alipokuwa akifanya kazi zake za nyumbani katika eneo la Moriema mjini Malindi Nchini Kenya.
Mashuhuda wa tukio hilo waliiambia polisi kuwa marehemu alikuwa amefungua mlango wa kuelekea kwenye kibaraza aliposhambuliwa na mbwa huyo aitwae wa Afrika Kusini maarufu kwa misuli yake iliyokua vizuri na umbile thabiti la mifupa.
Kulingana na mlinzi wa zamu wa usiku katika nyumba hiyo John Siria, alisikia mayowe ya mwanamke alipokuwa akishambuliwa na mnyama huyo, the star limeripoti.
Alisema alikimbia hadi eneo la tukio na kumzuia mbwa, kabla ya kumsaidia Nafuna aliyekuwa amelala sakafuni akivuja damu.
Kwa mujibu wa mlinzi huyo, marehemu alisema kuwa anajisikia ana nguvu na angerudi nyumbani peke yake.
Hata hivyo, mlinzi wa zamu ya mchana Anthony Katana, aliporipoti kazini alikuta mwili wa marehemu kwenye sakafu ya nyumba hiyo.
Maafisa wa upelelezi wa eneo la Malindi ambao walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kupata taarifa ya kisa hicho walibaini kuwa mwili wa marehemu ulikuwa na majeraha mengi yaliyotokana na kuumwa na mbwa huyo.
Uchunguzi wa tukio hilo la kusikitisha umeanzishwa huku mwili wa marehemu ukihamishiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha eneo hilo, ukisubiri uchunguzi zaidi.
Chanzo Bbc Swahili

Post a Comment