RAIS SAMIA ASHEREHEKEA MIAKA 62 YA KUZALIWA..AWAASA HAYA WATANZANIA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata keki kama ishara ya kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa leo tarehe 27 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
*****



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi Januari 27,2022 amesherehekea kumbukumbu ya miaka 62 ya kuzaliwa.


Akizungumza leo Katika mahojiano maalum ya kipindi cha Amka Tanzania kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Rais Samia Amewaasa Watanzania kujituma na kufuata mila, desturi, Katiba ya Nchi, taratibu na Sheria za nchi.


Amesema kuwa duniani kuna nchi moja inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ndani yake kuna Watanzania hivyo kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuijenga Nchi.


"Tufanye kazi kwa bidii ili tuinyanyue nchi yetu kwani nchi haijengwi na mtu mmoja."Amesema Rais Samia




Post a Comment

Previous Post Next Post