Wabunge 11 wa chama cha Conservative
Party nchini uingereza wamewasilisha barua za
kutokuwa na imani na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Boris Johnson.
Taarifa hiyo imeripotiwa na Gazeti la The
Telegraph na kuongeza kuwa kisheria
ni barua 54 za wabunge wa chama hicho zinazohitajika ili kutekeleza kura hiyo
isiyokuwa na imani kwa Johnson.
Kiongozi huyo aliichukua nafasi hiyo ya waziri mkuu mwaka 2019 ili
kuukamilisha mchakato wa Brexit kwa kushinda viti vingi katika kipindi cha
miaka 30.
Kwa sasa Boris anakabiliwa na shinikizo la kuachia ngazi baada ya
ufichuzi kuhusiana na sherehe za kunywa pombe zilizoandaliwa katika makazi na
afisi yake ya namba 10 Downing Street kipindi nchi ilipokuwa imefungwa kwa
ajili ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Johnson ameomba radhi mara kadhaa kuhusiana na sherehe hizo
akisema alikuwa hafamu zilipokuwa zikifanyika.
Chanzo Dw kiswahili
Post a Comment