Shabiki maarufu wa timu ya Taifa ya Mpira wa miguu ya Nchini Kenya "Harambee Stars" Isaac Juma mwenye umri wa miaka 56, anadaiwa kuuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Rukaya, Mumias, Kaunti ya Kakamega.
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Polisi (OCPD) wa Kaunti ya Mumias Magharibi, Stephen Muoni alithibitisha kifo cha Juma, na kuongeza kuwa mmoja wa washukiwa wawili amekamatwa kuhusiana na tukio hilo huku msako wa kumtafuta mwingine ukiendelea.
"Alikuwa nyumbani kwake aliposikia zogo kwenye zizi lake la kondoo. Akitoka nje pamoja na mwanawe na kaka yake watu hao wawili walimkatakata Juma hadi kufa huku mwanawe na nduguye waliponea chupuchupu," akaongeza OCPD.
Kwa upande wake Mke wa pili wa Marehemu ambaye ni Farida Juma amesema kuwa shabiki huyo maarufu aliuawa majira ya saa tisa chanzo kikiwa ni mgogoro wa Ardhi.
Katika mahojiano na televisheni ya Citizen nchini humo mwaka 2018, Marehemu Isaac alisema ana matumaini kwamba timu ya Kenya itafuzu kwa michi za Afcon ambazo kwa sasa zinaendelea nchini Cameroon.
Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakimkumbukakama jina lake maarufu-One, kama alivyofahamiwa na mashabiki wake.
Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakimkumbukakama jina lake maarufu-One, kama alivyofahamiwa na mashabiki wake.
Post a Comment