WAZIRI UMMY AITAKA MSD KUMALIZA CHANGAMOTO ZA UPATIKANAJI WA DAWA KATIKA VITUO NCHINI

 


Na WAF DAR ES SALAAM

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameiagiza Menejimenti ya MSD kutatua changamoto za upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za Afya nchini.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo wakati alipotembelea bohari ya dawa (MSD) kuongea na menejimenti kuhusu changamoto za upatikanaji wa dawa alizozipata kutoka kwa wananchi.


Waziri ummy amesema Lazima changamoto hii itatuliwe haraka iwekanavyo huku akisisitiza uwepo wa  dawa muhimu ambazo mwananchi anaandikiwa na daktari.

“Tutahakikisha upatikanaji wa dawa muhimu zote Katika vituo vya kutolea huduma za afya. Rais Samia Suluhu Hassan ametuwezesha kupata fedha za kununua dawa na hili nitalisimamia kikamilifu kuhakikisha zinanunuliwa na kusambazwa kwenye vituo kwa wakati". Amesema Waziri Ummy.


Aidha, Waziri Ummy ameendelea kuwasisitiza Watanzania kujiunga na mfuko wa taifa wa Bima ya Afya ili waweze kupata huduma za matibabu ikiwamo dawa bila kikwazo cha fedha.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amempongeza mkurugenzi wa MSD na timu yake kwa kufanya vizuri katika kusimamia uanzishaji wa viwanda vya ndani vya dawa na kuwataka kuendelea kubuni zaidi aina ya viwanda vitakavyozalisha bidhaa muhimu za afya ili kutatua changamoto za dawa na vifaa tiba nchini.

MWISHO

Post a Comment

Previous Post Next Post