Watoto wawili wa familia moja katika kijiji cha Usuhilo Mkoani Tabora, wamefariki dunia kwa kukosa hewa kutokana na moshi mzito uliotokana na jiko la mkaa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amewataja watoto hao kuwa ni Watoto waliofariki ni Amani Athumani mwenye umri wa mwaka mmoja na nuzu na Zainabu Athumani mwenye umri wa mwaka mmoja.
Kamanda Abwao amesema kuwa tukio hilo limetokea February 5, 2022 majira ya saa 6 usiku katika kijiji cha Usubilo kata ya Ifucha manispaa ya Tabora ambapo wazazi wa watoto hao waliwasha jiko la mkaa kwa ajili ya kujikinga na baridi hali iliyosababisha moshi mzito kutanda katika nyumba hiyo.
Amesema kuwa kutokana na kuwepo lwa madirisha madogo katika nyumba hiyo moshi huo uliwaathiri watoto hao na kupelekea vifo vyao.
"Walikuwa wamewasha moto na kutokana na miundombinu ya nyumba kuwa na madirisha madogo iliyosababisha watoto hao kufariki kutokana na kukosa hewa" amesema ACP Abwao
Wahanga wengine wa tukio hilo ni wazazi wa watoto hao akiwemo Athumani Shabani (45), Mkewe Magreth Joseph (34) pamoja na Neema Athumani (17) wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete kutokana na kuathirika na moshi huo na inaelezwa kuwa hali zao sio nzuri.

Post a Comment