Baraza la Taifa la Kudhibiti Ukimwi (NACC) Nchini Kenya limesema kuwa kuna uhaba mkubwa wa upatikanaji wa kondomu nchini Kenya hali inayowaweka wananchi katika hatari ya kuambukizwa VVU/UKIMWI, mimba zisizotarajiwa na magonjwa mengine ya zinaa.
Akizungumza wakati wa kuadhimisha Siku ya Kondomu Duniani katika Chuo Kikuu cha Kenya Coast Polytechnic mjini Mombasa Jana Jumapili Februari 13, 2022 Mratibu wa NACC Kanda ya Pwani Omar Mwanjama amesema kuwa nchi inakabiliwa na upungufu wa kondomu milioni 401, hatua ambayo imeathiri ugavi wa bure wa bidhaa hiyo kwa watu wanaolengwa.
Amesema kuwa mahitaji ya kondomu nchini yanafikia milioni 480 kila mwaka huku akiba ya sasa ikiwa ni milioni 79 pekee.
“Nchi inajitahidi katika kushughulikia upatikanaji wa chini ikilinganishwa na mahitaji Uhaba huo ni wa kweli na unahitaji kutatuliwa kwani unaweza kupunguza kasi ya mafanikio katika mapambano dhidi ya Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa,” alisema Mwanjama.
Amesema kuwa upungufu huo wa Kondomu umeilazimu NACC kuzingatia tu wale wanaohitaji sana bidhaa hiyo inayotolewa bure na serikali.
“Hali imetulazimisha kuzingatia wale tu wenye uhitaji mkubwa, jambo ambalo limezua malalamiko.
Upungufu wa Kondomu unatokana na kuwa idadi kubwa ya watu inategemea kondomu za serikali.
Post a Comment