Ndani ya moja ya majengo yanayoheshimika sana duniani - makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani.
Wataalamu wa picha na mafundi wamevaa glovu mikononi kuhakikisha mchoro huu wa kihistoria haupati madhara kwa namna yoyote ile. Watu wengine wawili wanafuata kwa ukaribu wakiwa wabeba mablanketi kuhakikisha wanayatanguliza chini sakafuni ikiwa wabebaji watalazimika kuuweka chini mchoro. Mchoro huu mkubwa wenye urefu wa mita 3.5 sawa na (futi 11) na upana wa mita 7.8 sawa (futi 25.6), umebebwa na watu wanne.
Picha hii ambayo inaonesha watu wakihangaika na matokeo ya vita, inatundikwa katika ukuta wa ukumbi wa Baraza la Usalama kwa umakini mkubwa. Kuna mtu ameshika karatasi yenye picha ya awali mchoro huo ulivyokuwa umetundikwa ili watundikaji wapya wasifanye makosa. Nao pia wana vifaa vya kupima kila nukta ya urefu kwenye ukuta.
Mnamo mwezi Februari mwaka jana 2021 wakati mchoro huu ulipochukuliwa, vyombo vya habari vilimnukuu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akionesha masikitiko yake. Lakini pia sasa imefahamika kuwa Katibu Mkuu Guterres mwishoni mwa mwaka jana baada ya kupata habari kuwa mchoro huo ungerejeshwa, aliandika barua Desemba 15, 2021 kwa Bw. Rockefeller akisema, “Hizi ni habari nzuri sana tunapomaliza mwaka mgumu wa matatizo na mizozo duniani. Picha ya Guernica inazungumza na ulimwengu kuhusu hitaji la dharura la kuendeleza amani na usalama wa kimataifa. Tunayo heshima ya kutumika kama wasimamizi makini wa kazi hii ya kipekee - tunapopata hamasa kutoka kwenye ujumbe wake."
Familia ya Rockerfelleller kupitia Nelson A. Rockefeller, Jr inaushukuru Umoja wa Mataifa kwa kuutunza mchoro huu lakini pia wanalenga kuwa hapo baadaye mchoro itabidi uzunguke katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu ili watu wengi zaidi wapate kuuona na kuutafsiri ujumbe wake ili kuitunza amani ya ulimwengu kama alivyolenga mchoraji Picasso mwenyewe takribani miaka 87 iliyopita.
MCHORO WA KIHISTORIA WA PICASSO UNAOFAHAMIKA KAMA GUERNICA WAREJESHWA
MWANZA DIGITAL
0
Post a Comment