Miili ya watu watatu ambao ni waendesha pikipiki maarufu bodaboda imeokotwa katika msitu ya Kijiji cha Hiari Mkoani Mtwara.
Akithibitisha hayo jana Jumanne Februari 15, 2022 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema kuwa tukio la kwanza limetokea katika Kijiji cha Hiati ambapo viliokotwa viungo vinavyodhaniwa kuwa vya binadamu ambavyo ni mifupa, ugoko na utumbo mdogo vinadhaniwa kuwa ni vya mwendesha bodaboda, Kelvin Mbale ambaye alitoweka tangu Februari 2, 2022.
Kamanda Katembo amesema katika eneo la tukio zilipatikana nguo na viatu ambapo ndugu za walivitambua kuwa vilikuwa vya marehemu.
Katika tukio la pili Kamanda amesema kuwa linahusisha mauaji ya Mohamed Juma anayedaiwa kuuawa na watu wasiojulikana kwa kuchomwa kitu chenye ncha kali.
Amesema tukio hilo limetokea Februari 12, 2022 katika huko maeneo ya pori la Majengo Wilaya ya Mtwara.
Amesema kuwa taarifa zinaonyesha kuwa Juma alipakia watu wawili wakiwa na mabegi mgongoni na kuelekea kusikojulikana na baadaye bodaboda wenzake walianza kumtafuta maeneo kukukuta mwili wake katika pori hilo.
Mwili huo umepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara ya Ligula kwa ajili ya kuhifadhiwa huku ukisubiri ndugu wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi.
Katembo amesema Februari 15, 2022 Polisi walipokea taarifa ya kupatikana kwa mwili mwendesha bodaboda, Mohamed Juma Mohamed (22).
Kaimu Kamanda wa Polisi Mtwara amesema upelezi wa matukio hayo unaendelea kuwabaini wote waliohusika na mauaji hayo.
"Jeshi la Polisi mkoani hapa linaendelea na msako, operesheni na ukusanyaji wa taarifa za kiitelijensia kukomesha aina zote za uhalifu" amesema Katembo.
Taarifa za awali kutoka kwa waendesha bodaboda katika maeneo mbalimbali ya halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani zinadai kuwa kuanzia Januari mwaka huu waendesha bodaboda nane wamepotea baada ya kukodiwa na watu wasiojulikana.
Mwisho
Post a Comment