Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka wadau wanaopendekeza matumizi ya viberenge katika kupanda Mlima Kilimanjaro kutathimini kwa kina mpango huo ambapo ameonyesha kutoridhia mikakati hiyo.
"Nasikia mnataka kuweka kiberenge cha kupanda Mlima Kilimanjaro, mnataka kuua mlima? Mkiweka machuma ya kupanda mlima mtaharibu, nataka mje mseme wapagazi mtawapeleka wapi na hizo ndiyo ajira zao, endeleeni kulijadili hilo mje na sababu zilizo tosha,” amesema Waziri Mkuu.
Ameyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa akiwa Chuo Cha Ushirika Moshi katika kilele cha mbio za Kilimanjaro Marathon mkoani Kilimanjaro, leo Jumapili Feb.
Post a Comment