Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali katika Wizara ya Maji, Nishati na Madini.
Kupitia taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Februari 11, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena Said amesema kuwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua ndugu Maryam Issa Juma kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti.
Pia amemteua ndugu Mwanamosi Ali Mwinchande kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utumishi na Uendeshaji.
Post a Comment