Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alikataa ofa ya Washington ya kumsaidia kuondoka Ukraine, vyombo vya habari vya Marekani vinasema.
"Mapambano yamefika. Nahitaji risasi, sio msaada wa kuondoka", shirika la habari la Associated Press lilisema, likimnukuu afisa mkuu wa kijasusi mwenye ufahamu wa moja kwa moja wa mazungumzo hayo.
Gazeti la Washington Post pia lilikuwa limewataja maafisa wa Marekani na Ukraine ambao walisema kuwa serikali ya Marekani iko tayari kumsaidia Bw Zelensky.
Bw Zelensky amesifiwa sana kwenye mitandao ya kijamii kwa jibu lake kwa uvamizi wa Urusi. Mchekeshaji na mwigizaji huyo wa zamani hapo awali alitoa hotuba ya kusisimua ambapo aliapa kuendelea kupigana, akisema: "Unapotushambulia, utaona nyuso zetu. Sio migongo yetu."
Pia alikuwa amechapisha video ya kujipiga mwenyewe mapema Ijumaa ikimuonyesha yeye na wasaidizi wake wakuu katika mji mkuu, akipinga ripoti kwamba alikimbia Kyiv.
"Sote tuko hapa," alisema. "Na itakaa hivi."
Post a Comment