Serikali Kupitia Wizara ya Nishati imeondoa Tozo ya Tsh. 100 kwa kila lita ya Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa, zilizopaswa kulipwa na watumiaji wa mafuta nchini kwa muda wa miezi mitatu zaidi kuanzia Machi 20 hadi Mei 2022 huku ikiendelea kutathmini mwenendo wa bei za mafuta.
Kutokana na kuendelea kupanda kwa bei za mafuta katika soko la dunia kunakosababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo vita kati ya Urusi na Ukraine, mwenendo wa bei za mafuta nchini umeathirika kwa bei hizo kuendelea kupanda.
Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Nishati imeelezwa kuwa uamuzi huo utaipunguzia Serikali mapato ya kiasi cha Shilingi bilioni 30 kwa mwezi.
Post a Comment