Na Samir Salum
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliamo Ikulu leo Ijumaa Februari 11, 2022 amesema kuwa Rais Samia ameshuhudia utiaji saini wa baadhi ya mikataba na makubaliano baina ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania, Mwigulu Nchemba na Waziri wa Biashara wa Ufaransa Frank Reister.
Miongoni mwa makubaliano hayo ni mkataba
wa mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 178 kwa ajili ya kugharamia
mradi wa ujenzi wa barabara wa mabasi yaendayo haraka.
Serikali hizo pia zimesaini mkataba wa
mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 80 ili kuimarisha Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kufikia malengo ya kutoa mikopo ya muda mfupi
na mrefu kwa sekta ya kilimo.
Aidha Rais Samia ameshuhudia utiaji saini wa mikataba mingine ya ushirikiano baina ya nchi hizo iliyosainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula kwa niaba ya serikali
Pia zimesaini tamko la dhamira ya kushirikiana katika eneo la uchumi wa buluu na usalama wa bahari.
Awali Rais Samia amehutubia katika mkutano wa 'One Ocean Summiť mjini Brest, Ufaransa, ulioandaliwa na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa
Katika mkutano huo ameyasihi mataifa yote kuheshimu makubaliano na maazimio waliyotia saini, kama wajibu wa kuchukua hatua madhubuti katika kulinda bahari.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya Tanzania na Ufaransa iliyosainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula pamoja na Waziri wa Biashara wa Ufaransa Frank Reicster katika mji wa Brest nchini Ufaransa leo Ijumaa Februari 11, 2022.
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya Tanzania na Ufaransa iliyosainiwa na Mkurugenzi mtendaji wa TADB Franck Reicster pamoja na Mwakilishi wa Serikali ya Ufaransa katika mji wa Brest nchini Ufaransa leo Ijumaa Februari 11, 2022.
Post a Comment