WAJUMBE WA BODI YA UDHAMINI WAMGOMEA ABRAMOVICH.


Wajumbe wa Bodi ya Udhamini wa Klabu ya Chelsea, bado hawajakubali maombi ya bilionea na mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich kuhusu kukabidhiwa majukumu ya kuiongoza timu huku yeye akibaki kuwa mmiliki.

Inaelezwa kuwa wajumbe saba akiwemo Kocha wa Chelsea ya Wanawake, Emma Hayes walijulishwa mpango huo wa Abramovich dakika chache kabla haujatangazwa, juzi Jumamosi lakini hawakukubali kwa kuwa wanahitaji taarifa zaidi.

Wajumbe hao walifika klabuni kujua kinachoendelea na kwa namna gani watafanya kazi kama ambavyo wameombwa. Hofu yao kubwa ni kuwa wasije wakaonekana wanataka kuitumikia klabu kutimiza malengo yao wakati huu ambapo bilionea huyo anajiweka pembeni katika mamlaka ya kutoa maamuzi ya utendaji wa klabu.

Vyanzo kutoka ndani ya Chelsea vinaeleza kuwa licha ya kuwa hadi sasa bado mambo hayajakaa kwenye mstari lakini kuna uwezekano wa kuelewana siku chache zijazo.

Abramovich alitangaza kujiweka pembeni Februari 25, 2022 kutokana na presha kuwa kubwa kwa sababu ya urafiki wake na Rais wa Urusi, Vladimir Putin ambaye taifa lake linaishambulia Ukraine kijeshi.

Post a Comment

Previous Post Next Post