WALINZI WA BAR WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KIJANA ALIYESHINDWA KULIPIA SHILINGI 1000 YA POMBE


Jeshi la Polisi Mkoani Kigezi Nchini Uganda wanawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji kufuatia kifo cha kijana mmoja aliyeuawa baada ya kudaiwa kushindwa kulipa Shilingi 1,000 (700Tsh) ya pombe.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Mkoani Kigezi, Elly Maate alimtaja marehemu kuwa ni Fred Ainembabazi Obadia mwenye umri miaka 23.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Ambrose Ensinikweri, Harriet Bagasheki na Nancy Komugisha ambao ni walinzi wa baa wote wakazi wa Karukata Trading Centre iliyopo kata ya Nyarushanje Wilaya ya Rukungiri Nchini Uganda.

Msemaji huyo wa Polisi amesema Obadia aliagiza pombe aina ya yenye thamani ya pesa ya uganda shilingi 1,000 (700Tsh) kutoka kwa baa ya Komugisha lakini akashindwa kulipia na kujaribu kutoroka.

Amesema kuwa Mashuhuda waliliambia Jeshi la Polisi kuwa walinzi wa baa walimfuata Obadia ambaye alinaswa nyumbani kwa Bagasheki katika Kijiji cha Bugarama ambapo walimfunga kwenye mti na kumpiga hadi kupoteza fahamu.

Ameongeza kuwa Fred aliokolewa na Polisi na kukimbizwa katika Hospitali ya Misheni ya Kisizi ambapo alipoteza maisha.

Aidha Msemaji wa Polisi ametoa wito kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa ili jeshi la polisi lichuku hatua stahiki.

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post