WASIO NA AJIRA KULIPWA KILA MWEZI NA SERIKALI- ALGERIA



Serikali Nchini Algeria anasema kuwa itaanzisha mafao ya ukosefu wa ajira kwa vijana wakati nchi hiyo ikipambana na ukosefu wa ajira uliokithiri.

Kauli hiyi imetolewa na Rais Abdelmadjid Tebboune wa nchi hiyo jana Jumanne Februari 15, 2022 wakati akihojiwa na kituo cha televishen cha Nchi hiyo ambapo amesema kuwa zaidi ya watu 600,000 Nchini humo hawana ajira.

Rais Tebboune amesema kutokana na changamoto hiyo serikali itaanza kutoa mafao kuanzia Mwezi March, 2022 kwa vijana wasio na kazi wenye umri kati ya miaka 19 hadi 40.


Amesema kuwa vijana wasio na kazi watakuwa wakilipwa dinari 13,000 kwa mwezi (karibu dola 100) pamoja na baadhi ya mafao ya matibabu, hadi wapate kazi.

Mnamo Novemba, wabunge walipiga kura kufuta ruzuku kubwa ya serikali kwa bidhaa za kimsingi ambazo kwa muda mrefu zimesaidia kudumisha amani ya kijamii, lakini hiyo ilidhoofisha bajeti za serikali huku mapato ya nishati yakipungua.

Wakati huo huo, kiongozi huyo wa Algeria pia alisema kuwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu utafanyika katika robo ya nne ya mwaka huu, baada ya hapo awali kutangaza kuwa utaahirishwa.

Mkutano wa 31 wa Umoja wa Nchi za Kiarabu ulipangwa kufanyika mwezi Machi baada ya Tebboune kusema kuwa nchi yake itakuwa mwenyeji mwezi wa Novemba. Tarehe mpya ya mkutano itatangazwa mwezi ujao.

Post a Comment

Previous Post Next Post