Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) linamshikilia ALLEN SAMWEL MHINA, Miaka 31, Mbondei, Mkurugenzi wa Mtandao wa kijamii wa U-turn Collection mkazi wa Temeke Mwembeyanga na wenzake 13 kwa tuhuma za kusambaza video katika mitandao ya kijamii kinyume na sheria.
Katika video hiyo imemuonyesha mmoja wa wagonjwa aliyekuwa amelazwa wodi ya ICU Hospitali ya Taifa ya Muhimbili suala lililoleta taharuki kwa Hospitali hiyo na wafanyakazi wake.
Watuhumiwa hao walikutwa na vifaa mbalimbali vya kieletroniki vya kiuchunguzi ambavyo ni Kamera, Kalamu, Saa Funguo, Miwani, Kofia, Laptop, Memory Card ambavyo vyote vinachunguzwa.
Kitendo kinachotuhumiwa kufanywa na watuhumiwa hao kililenga kudhalilisha, kutia hofu au kuleta taharuki suala ambalo linalazimisha mamkala hizi mbili za kisheria kuchunguza kwa kina suala hilo. Uchunguzi ukikamilika watafikishwa kwenye vyombo vingine vya kisheria.
Imetolewa na
MULIRO J MULIRO– ACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
======
Hivi karibuni kuliibuka skendo ya msanii na mwanasiasa Profesa Jay kupigwa picha akiwa chumba cha ICU, Muhimbili, tukio ambalo lilizua taharuki na kusababisha kutolewa kwa matamko kadhaa, ikiwemo kufanyika kwa uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Post a Comment