Kiasi cha shilingi Bilioni 26.6 zimetumika kwaajili ya kukamilisha mradi wa kisasa wa stend ya mabasi na malori Nyamhongolo wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masalla wakati akizungumza na washiriki wa mbio za Ilemela maarufu Ilemela Jogging Clubs zinazojumuisha virabu mbalimbali vya mbio vinavyopatikana mkoa wa Mwanza vikiwemo Lake Zone Runners, Wasafi Jogging, EFM Jogging, UVCCM Jogging na wananchi wengine ambapo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwaajili ya Utekelezaji wa mradi huo huku akiwaasa wananchi kuutunza na kutumia fursa za kiuchumi zinazotokana na uwepo wa mradi huo ikiwemo vizima vya biashara
'.. Huu ni mradi mkubwa wa stendi ya kisasa Afrika Mashariki inayopatikana wilaya ya Ilemela, Zimetumika zaidi ya Bilioni 26.6 kukamilisha kwake niwaombe tujitokeze kutumia fursa zitakazopatikana ..' Alisema
Aidha Mhe Masala amempongeza Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni Waziri wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula kwa ushirikiano wake katika kuhakikisha mradi huo unakamilika
Kwa upande wake mtaalam kutoka Manispaa ya Ilemela Ndugu Ahmed Sakibu amesema kuwa matangazo kwaajili ya wananchi kujitokeza kuanza kuomba vizimba vya biashara na maduka makubwa ya kisasa yataanza kutolewa kuanzia siku ya Jumatatu kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii hivyo kuwaasa wananchi kujitokeza kuomba fursa mbalimbali za kiuchumi zitakazopatikana sanjari na kuwaomba kuutembelea mradi huo wakati wowote kabla ya kuanza kutumika rasmi
Fadhili Ramadhan ni Moja ya wananchi waliojitokeza katika kushiriki mbio za Kilomita nane zilizoanzia Buzuruga na kuishia Nyamhongolo stendi ambapo amempongeza Mkuu wa wilaya ya Ilemela Kwa ubunifu wake katika kuhamasisha mbio hizo kwani mbali na kusaidia katika kupambana na magonjwa lakini pia zimeanza kutumika kwaajili ya kujikwamua kiuchumi Kwa kuhakikisha wananchi wanashirikishwa katika kutambua fursa za kibiashara na uchumi
Wilaya ya Ilemela inaendelea na Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo ya sekta ya afya, Elimu, miundombinu ya Barabara, Maji na huduma nyengine za kijamii
Post a Comment