GHALA LETU LA DODOMA LINAUWEZO WA KUTUNZA TANI 12,000 ZA CHAKULA KWA WAKATI MMOJA-WFP

 SHIRIKA la Mpango wa Chakula Duniani(WFP) limesema ghala lake la kuhifadhi chakula lililopo Dodoma lina uwezo wa kutunza tani 12000 za chakula kwa wakati mmoja.

Pia limesema pamoja na majukumu yao mengine, WFP wamekuwa na jukumu la kupokea, kutunza na kusafirisha chakula kwenye kambi za wakimbizi zilizopo Kigoma na nchi jirani ikiwemo Sudan Kusini.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini ambavyo vimefanya ziara ya kutembelea ghala la kuhifadhi chakula la WFP-Dodoma, Meneja wa ghala hilo Elianami Rushatsi amesema ghala hilo lina uwezo wa kuhifadhi tani 12000 kwa wakati mmoja.

"Ghala letu la kuhifadhi chakula la Dodoma lina uwezo wa kutunza tani 12,000 kwa wakati mmoja, chakula tunachotunza kwa sasa kwa wingi ni Mtama , Mahindi na Mafuta.

Pia tunanya usagaji wa mahindi kwa ajili ya chakula cha kupeleka katika kambi ya wakimbizi huko Kigoama,"amefafanua.

Rushatsi amesema katika ghala la chakula Dodoma pia wamekuwa wakifanya usagaji ambapo kwa siku wana uwezo wa kusaga tani 120 kwa kutumia mashine tatu walizonazo.

"Kwa hivi sasa tunasaga tani 80.Pia kuna baadhi ya kazi zetu tumezipa kampuni nyingine kufanya kwa niaba yetu,kampuni hizo zimeingia na mktaba na WFP.

"Kwa mfano kuna kampuni inayopakia na kupakua mazao, kampuni nyingine inahusika na watu wa kufanya usafi, kwa hiyo hizo ni kampuni tofauti na WFP tumeingia nao mkataba kwa ajili ya kufanya kazi hizo.

Alipoulizwa chakula ambacho kimekuwa kikipelekwa kwenye kambi za wakimbizi kinatolewa nani, amesema kumekuwepo na wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakisaidia kutoa chakula kwa ajili ya kupelekwa kwa watu wenye uhitataji wakiwemo wakimbizi katika kambi ya Kigoma.

Sehemu ya chakula kikiwa kimehifadhiwa katika mifuko maalum katika Ghala la kuhifadhi chakula la Shirika la Mpango Duniani(WFP) .Ghala hilo limekuwa likitumika kupokea,kutunza na kusafirisha chakula katika maeneo yenye uhitaji ikiwemo kambi ya wakimbizi Kigoma.

Sehemu ya muonekano wa mashine ya kusaga

Meneja wa Ghala la kuhifadhi chakula la WFP-Dodoma Elianami Rushatsi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari ( hawapo pichani) kuhusu uwezo wa mashine zinazotumika kusaga mazao

Muonekano wa nje wa Ghala la kuhifadhi chakula la WFP- Dodoma ambapo kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani ghala hilo linauwezo wa kutunza tani 12000 za chakula kwa wakati mmoja

Meneja wa Ghala la Chakula la WFP- Dodoma Elianami Rushatsi akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea kwenye ghala hilo kubwa la kuhifadhi chakula.


Post a Comment

Previous Post Next Post