Hii ni Sehemu ya nukuu za Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Machi 18, 2022:
Tume hii ya leo imepeleka majina bungeni ya kughushi na watu wameapishwa kuwa wabunge, halafu mnakuja mnasema turidhiane sasa tunalidhiana kwa lipi? Lazima tuzungumze kwanza kilichosababisha turidhiane."
"Kongamano la TCD tumeshauriana kama chama, haya maridhiano yanayozungumzwa kupitia TCD sisi hatukushiriki kuyaandaa na sisi hatutashiriki kongamano la TCD na hatuoni njia ya kupata katiba mpya kupitia TCD, siyo Mbowe wala chama kitakachoshiriki kongamano hilo."
"Tumeumizwa sana, tunakubali maridhiano na mazungumzo ni jambo jema. Ila kabla ya kwenda kuridhiana lazima tuulizane tuliitarifiana wapi? Tulikosana wapi? Wengine hata hawajashiriki chaguzi, hawajaumizwa wanasema turidhiane sasa tunaridhiana na nini?"
"Nilitambua kiu na shauku ya Watanzania wengi wakitaka kusikia kauli ya Mbowe, kimsingi kauli ya Mbowe ni kauli ya chama, hivyo isingekuwa sahihi kama kauli ya Mbowe ingetoka bila ya Mbowe kukaa na chama chake."
"Nilichokubaliana na Rais Samia Suluhu kimsingi ni jambo moja tu, kutafuta haki kupitia mazungumzo na mshauriano ili kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili Taifa letu."
"Kamwe hatutaweza mapambano ya kutafuta uhuru na ustawi wa watu huku tuwe na chuki au kisasi. Kisasi sio azma ya Mbowe au CHADEMA na azma hiyo naithibitisha kupitia siku zangu nilizokuwa gerezani.”
"Nimesema na ninasema kuwa, natangaza msamaha kwa yeyote yule nafikiri aliyenitendea baya, sina chuki wala kisasi na nawaomba Wanachadema wenzangu tusiwe na chuki na yeyote katika mapambano ya kutafuta uhuru na Ustawi wa watu.”
"Nimekuwa gerezani kwa muda mrefu na nimejifunza mengi sana, nataka kuwahakikishia Watanzania na dunia kuwa sikupoteza zile siku.”
"Hakika nimeushuhudia upendo na sijui kwamba nitaulipa kwa njia gani, na nimekuwa nikilizungumza hili kila nikipata nafasi, siku zangu na walinzi wangu tukiwa gerezani, dunia ulisimama upande wetu kwa mithili na mifano ambayo siwezi kuielezea.”
"Chini ya mbingu kila jambo lina wakati wake, kuna wakati wa kukusanya na kuna wakati wa kutawanya, na mengine mnaweza kusoma katika biblia kwenye kitabu cha Muhubiri mlango wa 3."
"Nilitambua kiu na shauku ta Watanzania wengi wakitaka kusikia kauli ya Mbowe, kimsingi kauli ya Mbowe ni kauli ya chama, hivyo isingekuwa sahihi kama kauli ya Mbowe ingetoka bila ya Mbowe kukaa na chama chake."
"Leo nazungumza na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza baada ya miezi saba na nusu ya kuwa kifungoni. Waandishi mbalimbali walinitafuta kutoka vyombo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi wakitaka mwenyekiti nitoe kauli ya mambo kadha wa kadha yanayojiri katika nchi yetu lakini nilichelea kufanya hivyo."
"Baadhi ya wale waandishi wa habari walionifikia niliwaambia kila jambo chini ya mbingu lina wakati wake. Nilitambua kwamba kuna kiu na shauku kubwa ya Watanzania kusikia kauli ya Mbowe. Lakini kauli ya Mbowe ni kauli ya Chama. Isingekua sahihi kauli ya Mbowe ikatoka kabla Mbowe hajakaa na chama chake."
"Kwa hiyo nikawaambia chini ya mbingu kila jambo lina wakati wake. Kuna wakati wa kukusanya na kuna wakati wa kutawanya. Basi na mengine mkayasome kwenye Biblia kitabu cha Mhubiri mlango wa tatu."
"Nimesema na nasema tena, natangaza msamaha kwa yeyote ambaye nafikiri alinifanyia baya. Sina chuki wala sina kisasi."
"Nawaomba WanaChadema wenzangu tusiwe na chuki na yeyote katika mapambano haya kwa sababu mapambano haya ni kupigania uhai wa watu, ni kupigania ustawi wa watu. Kamwe hatuwezi kutafuta ustawi wa watu wakati tunatafuta visasi. Visasi sio utamaduni wa chadema,sio utamaduni wa Mbowe.
"Kwa hiyo mimi nimetoka na roho nyeupe kabisa, tukiwa tayari kwa kuendeleza kazi ya siasa."
"Nililetewa salamu za mheshimiwa Rais kwamba angependa kukutana na mimi mapema iwezekanavyo.
Mtakumbuka kwa muda mrefu sisi kama chama tulitaka kuzungumza na Rais tukiamini kwamba ana majibu ama ana ufunguzi wa mambo mengi yanayolisibu taifa letu."
"Kwa bahati mbaya hatukupata nafasi ya kukutana naye hadi ninakwenda gerezani. Kwa hiyo nikiwa gerezani siku natoka nikaambiwa kwamba mheshimiwa Rais angependa kukuona haraka. Nimetoka gerezani kwa moyo mweupe, wala sikutoka na kiburi, cha kwamba naweza nikapuuza mualiko wa Rais."
"Mbowe aliyeingia gerezani ndiyo Mbowe aliyetoka gerezani, tena pengine akiwa imara zaidi. Kwa hiyo nimezungumza na Rais mambo kadhaa. Lakini sikuyafikisha kwa umma kwa sababu nilihitaji kwanza kuzungumza na Kamati Kuu ya Chama changu na viongozi wenzangu."
"Nilipokwenda gerezani, chama hiki hakikuenda gerezani. Viongozi wenzangu walikuwepo, vikao vya chama vilifanyika, mashauriano mbalimbali yalitokea. Ninaporejea kutoka gerezani ninapaswa kwanza kukabidhiwa kiti changu ndo nizungumze kama msemaji mkuu wa chama."
"Kwa hiyo nawashukuru viongozi wenzangu walikilinda chama chetu katika mazingira magumu sana. Kwa hiyo ilinipasa mimi kwanza nizungumze na kamati kuu ya chama changu ili nitakapotoa kauli kwa umma nitoe kauli ya chama na sio kauli ya Mbowe."
"Waheshimiwa viongozi, nilipokwenda kukutana na mheshimiwa Rais Ikulu, tulichokizungumza ni kitu kimoja tu cha msingi. Kwamba tulikubaliana kutafuta njia za haki, za mazungumzo, za mashauriano katika kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili taifa letu."
"Hatukuenda kuzungumza hoja yoyote, moja baada ya nyingine. Kwamba nchi hii tukubaliane ni yetu sote, wao wapo kwenye uongozi na utawala wa taifa, sisi ni chama kikuu cha upinzani, na kuna Watanzania wengine ambao sio wanachama wa vyama hivi lakini ni Watanzania wenzetu."
"Na tulikubaliana kwamba tuna tatizo moja kubwa la kutokuaminiana kwa sababu tumekuwa na urafiki wa mashaka. Tumekua na urafiki wa mashaka na hakika tuna urafiki wa mashaka, hatuaminiani."
"Tukakubaliana, ili kuvuka kikwazo hicho, lazima kila upande ujaribu kujenga kwa mwenzake, na majibu yatapatikana kwa wakati, sio jambo au tukio la siku moja. Hilo lilikua la kwanza la msingi."
Post a Comment