PUTIN APATA PIGO,MSHAURI WAKE AJIUZULU..

Pamoja na kukwama kwa wanajeshi wa Urusi kusonga mbele vitani nchini Ukraine , Rais Putin anaonekana amepata pigo kutoka ndani ya Kremlin yenyewe.

Mmoja wa washauri wake, Anatoly Chubais, amejiuzulu kutoka jukumu lake kama mjumbe wa kimataifa - afisa mkuu zaidi kujiuzulu tangu kuanzishwa kwa uvamizi.

Ripoti za Urusi zilisema kwa sasa yuko Uturuki na mkewe
Bw Chubais alipewa kazi ya kuratibu malengo ya maendeleo endelevu ya Urusi kimataifa.

Baada ya vita kuanza alichapisha picha ya kiongozi wa upinzani aliyeuawa, katika kile kilichoonekana kama ishara mbaya.

Hakukuwa na maoni yoyote ya kuandamana na picha yake ya Facebook ya Boris Nemtsov, katika kumbukumbu ya kuuawa kwake kwa mtazamo wa Kremlin. Pia hajatoa maoni yoyote kuhusu kujiuzulu kwake.

Chanzo kimoja kililiambia shirika la habari la Tass kuwa ameondoka Urusi na pia kujiuzulu uwakilishi maalum wa Rais Putin.

"Ndiyo, Chubais amejiuzulu kwa hiari yake mwenyewe. Lakini ikiwa ameondoka [Urusi] au amebaki, hilo ni jambo lake binafsi," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema.

Post a Comment

Previous Post Next Post