Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble ametaja kifo cha Amina Mohamed Abdi kama "mauaji".
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo ametuma ujumbe wa rambirambi kwenye ukurasa wake wa Twitter:
Wahasiriwa wengine ni pamoja na mbunge wa zamani Hassan Dhuhul na wanajeshi wa Somalia.
Ripoti za vyombo vya habari nchini zinaonyesha kuwa idadi ya waliofariki inaweza kuwa kubwa zaidi.
Televisheni ya Taifa ya Somalia imetuma picha za wahasiriwa waliouawa katika shambulio hilo kwenye mtandao wa twitter.
Mashambulio ya mabomu ya kujitoa muhanga huko Beledweyne yalitokea saa chache baada ya wanamgambo washirika wa al-Qaeda kuua takriban watu wanane, ikiwa ni pamoja na raia watano wa kigeni, katika shambulio kwenye Kambi ya Halane, ngome ya uwanja wa ndege ambayo ina ofisi za Umoja wa Mataifa na ujumbe wa kigeni.
Al-Shabab wamesema ndio waliohusika na mashambulizi ya Mogadishu na Beledweyne ya kati.
Wanamgambo hao walizidisha mashambulizi kote nchini Somalia huku taifa hilo la Pembe ya Afrika likiendesha uchaguzi ambao umecheleweshwa sana
Takriban watu 15, akiwemo mbunge mwanamke wa bunge la shirikisho la Somalia, waliuawa katika milipuko miwili ya kujitoa mhanga katika mji wa Beledweyne katikati mwa Somalia.
Post a Comment