Miili miwili kati ya mitatu ya watu iliyopatikana juzi Ijumaa ilikutwa ikielea katika Mto Yala Nchini Kenya.Mmoja ulikutwa umetobolewa macho huku ukiwa umekunjwa na kitambaa katika mdomo, mwingine ukiwa umezungushiwa nailoni juu ya kichwa na kufunika uso.
OCPD Charles Chacha wa Yala amethibitisha kupatikana kwa miili hiyo ambayo ilikuwa imekwama kwemue miamba ndani yam to maeneo ya Kina.
Miili hiyo iligunduliwa na mfugaji ambaye alikuwa amepela mifugo yake kunywa maji katika mto huo.
Ugunduzi huo unafikisha jumla ya miili 29 iliyogunduliwa katika mto huo tangu Oktoba mwaka jana. Kufikia sasa, familia 12 tayari zimetambua jamaa zao kutoka mochwari ya kaunti ndogo ya Yala na kuwazika.
Oyaro alikuwa ametoweka tangu Agosti 28 alipokuwa akisafiri kutoka Marsabit kuelekea Nairobi kwa gari la KWS.
Matokeo ya DNA Alhamisi iliyopita yalithibitisha mwili wa Oyaro, baada ya sampuli zinazolingana zilizokusanywa kutoka kwa mamake mapema mwezi huu.
Post a Comment