Msanii wa Bongofleva, Maunda Zorro amefariki dunia kwa ajali ya gari usiku wa kuamkia leo, Kaka wa marehemu ambaye pia ni Msanii wa Bongofleva Banana Zorro amethibitisha taarifa hizo na kusema hadi jana jioni alikuwa pamoja na Maunda kwenye msiba wa Rafiki yao lakini baadaye akapata taarifa kuwa Maunda amefariki.
"Nimezipata hizo taarifa ndio naelekea Hospitali ya Kigamboni, taarifa ni za kweli tulikuwepo kwenye msiba jioni ya leo wa rafiki yetu mwingine wa karibu, nilikuwa nae Maunda hadi jioni saa 11 hadi 12 nikarudi nyumbani kulala maana msiba ulikuwa Kigamboni na yeye anakaa Tuangoma, kwa taarifa zaidi (kuhusu msiba) ni hadi nikifika Hospitali"
"Chanzo cha kifo ni ajali ya gari, nimeachana na Maunda saa 12 jioni ajali amepata mida ya saa 4 usiku, ila sina uhakika sana (wa muda aliopata ajali) hadi nikifika Hospitali maana nilirudi nyumbani nikiwa nimechoka sana"
#RIP MAUNDA ZORRO
Post a Comment