RC MWANZA AKABIDHI PIKIPIKI 13 KWA MAMENEJA WA WAKALA WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI {RUWASA}

 

      

Na Paul Nenetwa 👇

    Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Amekabidhi Pikiki 13 Zilizotolewa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mameneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini {RUWASA) Zitakazosaidia Kuyafikia Maeneo Yaliyoko Vijijini na kutoa huduma inayostahili kwa Wananchi.



    Katika Hatua nyingine Mkuu Huyo wa mkoa Alimuagiza Meneja wa Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira vijijini {RUWASA} Mkoa wa Mwanza Kufanyia matengenezo ya Haraka pikipiki nane {8} ambazo ni mbovu ili Ziweze Kutumika Katika Kutoa Huduma kwa wananchi kwa urahisi.



Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini {RUWASA} Daudi Amlima Alisema pikipiki hizo zimetolewa ikiwa ni juhudi za serikali kutoa huduma Bora za maji kwa wananchi.

''Ikiwa ni juhudi za serikali kuhakikisha RUWASA kupitia vyombo vya watoa huduma za maji ngazi ya jamii Tunasimamia Skimu za Maji na kuhakikisha zinatoa huduma ya maji kwa wananchi wetu'' Alisema Daudi Amlima



Juhudi hizi za Serikali zinalenga kuhakikisha utoaji wa huduma za maji vijijini zinatekelezwa kwa Ufanisi wa Hali ya juu na Wananchi wananpata huduma kwa wakati ikiwemo kupelekewa huduma za Maji Pamoja kufanyiwa Matengenezo katika Miundo Mbinu ya maji iliyoko Vijijini.


Post a Comment

Previous Post Next Post