Umoja wa Club za Waandishiwa habari Tanzania {UTPC} Umefanya Mkutano na Waandishi wa habari za Mitandao ya kijamii , Redio na Magazeti ili kupitia, kujadili na kuthibitisha kanuni za maadili ya uandishi wa habari zitakazosaidia kuwepo kwa miongozo itakayowasaidia na kuwalinda waandishi katika utekelezaji wa majukumu yao ya ukusanyaji, uchapishaji na usambazaji wa maudhui yao kwenye jamii.
Mwenyekiti wa Umoja wa Club za Waandishi wa Habari Tanzania Abubakar Karsan Katika Mkutano na Waandishi wa Habari za mtandaoni, Redio, Magazeti na Televisheni wa kupitia na kuthibitisha kanuni za uandishi wa habari jijini Mwanza.
Waandishi wa Habari Mtandaoni, Redio, Magazeti na Televisheni wakiwa katika mkutano wa kupitia, kujadili na kuthibitisha kanuni za uandishi wa Habari uliofanyika jijini Mwanza.
Mratibu wa Mrad Afisa Miradi wa UTPC, Victor Maleko Ambaye ni Mratibu wa Mradi wa Ushirikiano kati ya UTPC na International Media Support {IMS} Akizungumza kuhusu umuhimu wa kanuni hizo ndani ya Tasnia ya Habari hasa Uandishi wa Habari za Mtandaoni, Redio, Magazeti na Televisheni.Picha ya Pamoja ya Waandishi wa Habari za Mtandaoni, Redio, Magazeti na Televisheni walioshiriki mkutano wa kupitia, kujadili na kuthibitisha kanuni za Maadili ya Uandishi wa Habari.
Post a Comment