Na Oscar Mihayo - Mwanza.
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Sahili Geraruma ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa ujenzi wa kituo cha Afya, kilichojengwa Kata ya Bulale ambacho kitatoa huduma bora na kupunguza Vifo vya akina mama na watoto.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho cha Afya Geraruma amesema ni vyema sasa watendaji kujidhatiti Ipasavyo katika utoaji wa huduma bora ili thamani ya ujenzi wa kituo hicho iendane na huduma bora inayokusudiwa kutolewa kwa wananchi.
''Sisi kama viongozi wa mbio za Mwenge tunaridhia kuzindua kituo hiki baada ya kufanya ukaguzi wa kina na sehemu ambayo inahitaji maboresho nimeelekeza watalaamu waweze kumalizia ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba vyote muhimu'' amesema Geraruma.Awali akisoma risala, Mganga mfawidhi wa kituo hicho Dk. Abubakar Rajabu amesema uzinduzi wa kituo hicho utakuwa na msaada mkubwa kwa akina mama waliokuwa wanatembea umbali mrefu kutafuta huduma bora ya kujifungua salama.Amesema kwa sasa uboreshaji wa kituo hicho utaweza kuwasaidia kufanya upasuaji kwa akina mama wenye uhitaji huotofauti na awali ambapo walilazimika kwenda vituo vinavyotoa huduma ya upasuaji kutokana na kituo hicho kutokuwa na huo uwezo.Kwa upande wake Khadija Omar ambae nimsaidizi wa Afisa Lishe Nyamagana amesema kwa sasa wamejipanga hasa kwa ushauri wa namna bora ya wanawake wenye ujauzito ambao wanashauriwa namna bora ya kutumia vyakula vyenye protini ili kuweza kuwalinda wajawazito hao kukosa damu wakati wa kujifungua.
Naye Hussina Hamis mama mjamzito amepongeza uzinduzi wa kituo hicho kwa kuwa sasa wanaweza kuwa na uhakika wa afya zao wao na watoto wao tofauti na hapo awali ambapo iliwalazimu kutafuta huduma ya kujifungua mbali na makazi yao.
Post a Comment