Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Imefanya kikao kazi na watoa Huduma wa Maudhui Ya Mtandaoni Kanda ya Ziwa kujadili Changamoto wanazokumbana nazo pamoja ikiwa ni Pamoja na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya Uandishi wa Habari hasa wanapokuwa wakichapisha Maudhui yao Mtandaoni.
Akifungua Kikao hicho Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Ziwa Mhandisi Fransis Mihayo Alisema Ipo hapa kubwa ya kufuata Sheria,kanuni na kuzingatia maadili ya uandishi wa habari za mitandaoni kwani wimbi la ukiukwaji wa maadili kwa baadhi ya watoa maudhui mitandaoni kutokuzingatia kanuni na maadili ya uandishi wa Habari.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa umoja wa Club Ya Waandishi wa Habari Mkoa wa mwanza (MPC) Ndg.Edwin Soko Alisema katika wasilisho lake lililolenga kuangazia vitisho vya kimtandao na ulinzi kwa waandishi wa habari hasa wa maudhui ya mtandaoni kuwa wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi mkubwa ili kulinda Amani ya Taifa pamoja na kuchukua Tahadhali kubwa wakati wa utekelezaji wa majukumu yao hasa katika habari za zinazojikita katika uchunguzi {investigative Story}
Aidha kanuni za maudhui mtandaoni za mwaka 2022 zinamtaka mtoa maudhui mtandaoni kujikita katika kutoa Taarifa/Habari zenye ukweli ambazo hazina mlengo wa kutoa Taharuki kwa wananchi Kama ambavyo kanuni hizo ziliwasilishwa na kwa wanahabari hao na Ndg. Joseph Kavishe ambae ni Afisa Sheria kutoka TCRA Mkoa wa Mwanza.
Post a Comment