Wataalamu kutoka Idara Mbalimbali ndani ya Halmashauri na Manispaa zote Nchini wametakiwa kushiriki ipasavyo kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ili kuikamilisha miradihiyo ikiwa katika ubora uliokusudiwa.
Hayo yamesemwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Sahili Gerarumo katika mbio za mwenge ndani ya wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza ambapo alisema Miradi mingi inakamilika ikiwa na mapungufu mengi {chini ya kiwango} kwasababu ya Ushiriki duni wa wataalamu walioko katika halmashauri na manispaa nchini kwenye kamati zinazoundwa kwaajili ya kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo.
Alisema wataalamu wengi wamekuwa wakiwaachia majukumu wanakamati ambao kwa asilimia kubwa huwa hawana utaalamu juu ya mradi unaotekelezwa huku akitoa mfano wa kamati za maendeleo katika utekelezaji wa miradi ya majengo ya shule ambapo kwa asilimia kubwa wamekuwa wakiachwa wanakamati wakiwemo walimu, watendaji na wenyeviti wa mitaa ambao kiuhalisia hutegemea zaidi miongozo na ushauri kutoka kwa wataalamu hao.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo ya ilemela Mwl. Hassan Masala Aliyapokea Maelekezo Aliyopewa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa huku Akiibuka akijichukulia ushindi kupitia miradi iliyozinduliwa, kukaguliwa na kuwekewe mawe ya msingi Kwani hakuna Mradi hata mmoja uliokataliwa na Wakimbiza mwenge kitaifa kupitia kiongozi wao Sahili Gerarumo.
Aidha Mwenge huo wa uhuru ndani ya wilaya ya Ilemela Ulikimbizwa kilomita 84.1 na Uliifikia miradi nane {8} yenye thamani ya zaidi ya sh. Bilioni 1.9 ikiwa miradi hii ni kutoka ndani ya kata 10 kati ya kata 19 zilizopo ndani ya wilaya hiyo ya ilemela na kati ya miradi iliyofikiwa na mwenge wa uhuru, miradi miwili (2) iliwekewa mawe ya msingi, huku miradi mitano {5} ikizinduliwa na Mradi Mmoja Ukikaguliwa.
Post a Comment