Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dr. Angelina Mabula amewapongezawatanzaniawanaomiliki ardhi kwaajili ya uwekezaji kwani uwekezaji wao unatoa Fursa za Ajira kwa vijana Wengine kitendo ambacho kinaisaidia serikali kupunguza ongezeko la watanzania wasiokuwa na ajira.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa kituo cha mafuta cha Ashico Oil Kilichopo Busweru Wilayani Ilemela jijini Mwanza Ambapo kituo Hicho Kilizinduliwa na Mwenge wa Uhuru Kupitia kiongozi wa mbio za mwenge huo kitaifa Sahili Geraruma , Dr Mabula Alitumia nafasi hiyo kuwaeleza wananchi kuhusu ulipaji wa kodi ya pango la Ardhi, kodi itakayowezesha kumsaidia Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kupanga mikakati na kutekeleza shughuli mbalimbali za kimaendeleo zitakazolenga kuwanufaisha wananchi kupitia kodi hizo.
Aidha Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Geraruma Aliipongeza Wizara ya Ardhi kwa Kuwapa Ardhi wawekezaji wazawa ambao wamejenga Mradi wa kituo hicho cha Mafuta ambacho kimejengwa kwaajili ya kutoa huduma ya mafuta kwenye vyombo vya vya moto wilayani humo na hata nje ya wilaya hiyo.
Geraruma Alilidhishwa na utekelezaji wa mradi huo kisha kuweka jiwe la Uzinduzi wa kituo hicho cha mafuta ambacho pia kimeweza kutoa ajira kwa baadhi ya vijana ambao ni wakati wa wilaya ya ilemela.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Sahili Geraruma akizungumza na wakazi wa ilemela jijini mwanza |
muonekano wa kituo cha Ashico Oil |
Post a Comment