HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA WAJA NA MPANGO WA KUNUSURU VIFO VYA AKINA MAMA NA WATOTO

 

KATIKA kuhakikisha Jiji la Mwanza linalinda Afya ya Mama na Mtoto, wamekuja na mpango wa kuboresha miundombinu ya Afya kwa kupanua Zahanati na kuwa vituo vya Afya kwa kila Kata.

 Kauli hiyo Imetolwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza,Seleman Sekiete Mbele ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Nyamagana ilipofanya ziara ya kuangalia utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye kada ya Afya.


“Kituo hiki cha Shadi Kata ya Luchelele kipo katika hali nzuri na matarajio yetu kuwa Mwishoni mwa Mwaka huu kitaanza kutumika na kupunguza hadha ya akinama walikuwa wakilazimika kwenda Hospitali ya Wilaya ya Butimba Kilomita zaidi ya 10,kufuata huduma ya uzazi salama,”amesema Sekiete.

 Sekiete pia emempongeza Mhe.Rais Samia kwa kutoa kiasi cha Sh.Milioni 100 kwa ajili ya uapanuzi wa jingo hilo,huku akieleza wanampango pia wa kulipa watu ili kuwahamisha na kuweka majengo mengi zaidi ili kuhakikisha wanapunguza vifo vya akina mama na mtoto kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya Afya pamoja na wataalam.

 


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyamagana Athuman Zebadayo amesema ameridhishwa na uboreshaji wa miumndombinu kutoka kwa Halmashauri na kuwataka kuongeza kasi ya ukamilishaji wa miumdombinu hiyo ili jamii inufaike na ilani ya CCM.


Kwa upande wake mama mjazito Grace Mwisa amesema upanuaji wa Zahanati  hiyo kuwa kituo cha Afya ni ukombozi Mkubwa wa akina mama wa eneo hilo kwani walipokuwa wakibeba mimba ilikuwa roho mkononi kutokana na kuwaza kama utapewa rufaa ya kwenda hospitali ya Butimba.

 

“Kwanza kutoka hapa hadi kufika huko ni gharama kubwa na hapo mgonjwa wako ama mzazi unakuwa unauhakika kama atafika salama ama atajifungulia njiani ndiyo maana nasema kiukweli ujio wa kituo hiki hapa tutakuwa na amani pindi tunapokuwa wajawazito,”amesema Grace.

Post a Comment

Previous Post Next Post