Taarifa kutokea Kenya zinaeleza kuwa Ndege aina ya Gulfstream 550 yenye nambari N708JH inayomilikiwa na FBI wa kitengo cha haki cha nchini Marekani, imetua jijini Nairobi jana.
Tetesi zinadai kuwa Ndege hiyo imewafuata wahalifu wawili wa kiwango cha juu ambao walitolewa kwenye kituo cha Polisi cha Kilimani jijini jioni ya jana.
Ndege hiyo inatarajiwa kuondoka leo ambapo wahalifu hao wanaosadikiwa kuwa ni raia wa Somalia watahamishiwa nchini Marekani.
Post a Comment