MAKONDA AOMBA KUPANGIWA KAZI NYINGINE..

 


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema kuanzia sasa hadi Januari 1, 2025 atakuwa amekamilisha kazi ya kuwanyoosha watumishi wa umma wasiokuwa wazalendo na wanaotanguliza masilahi yao binafsi.


Makonda amemwomba Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi kwenda kumwombea kwa Rais Samia Suluhu Hassan amvumilie kwa kipindi hiki cha miezi sita.

Amesema hayo leo Jumatatu, Juni 3, 2024 katika mkutano wa hadhara wa Dk Nchimbi uliofanyika Soko la Kilombero, Arusha Mjini.

"Nikuhakikishie katibu mkuu, watakula spana za kutosha,”amesema Makonda.
Pia, amesema na ikifika Januari 1, 2025 atakuwa amekamilisha kazi na kama kutakuwa na mkoa mwingine yuko tayari kupelekwa.

Makonda amesema:"Amekuta mkoa huo kuna watumishi wasiokuwa wazalendo, hawataki kujituma, sio wote ila wengi wao wanatumia masilahi yao binafsi, naomba kaniombee kwa Rais, anivumilie kidogo, mfunge masikio nipige spana ili haki za wananchi zipatikane."

Katika kusisitiza hilo, Makonda amesema:"Nitawanyoosha mpaka kieleweke na ikifika Januari 1, 2025 utakuwa mkoa wa mfano."

Amesema kuna zaidi ya Sh20 bilioni zinazoweza kurudi serikalini zilizotolewa ili kutekeleza miradi mbalimbali lakini hazijatumika pasi na sababu za msingi huku wananchi wakilia kukosa huduma za afya, maji na elimu na hayuko tayari kuona hilo likitokea.

Post a Comment

Previous Post Next Post