MSIGWA AKATA RUFAA NA WANAOTAKA NIHAME CHAMA WAHAME WAO KWANZA..

 

Aliyekuwa Mwenyekiti wa #CHADEMA Kanda ya Nyasa ambaye amemaliza muda wake na kushindwa katika Uchaguzi uliompa ushindi Joseph Mbilinyi (Sugu), Mchungaji Peter Msigwa amekata rufaa kupinga Uchaguzi huo akidai ulivurugwa


Akizungumza na Waandishi wa Habari, Msigwa amesema Uchaguzi huo ulitawaliwa na Mbinu Chafu ikiwa ni pamoja na Wasimamizi wa Uchaguzi kuwazuia Makatibu Watatu wa Mabaraza kupiga Kura kinyume na Katiba ya Chama hicho


Amesema "Kama CHADEMA tunalalamikia CCM kwamba wasimamizi wa Uchaguzi huwa hawatendi Haki tulitakiwa tuwe mfano, sasa kama mimi mjumbe wa Kamati Kuu ninatoa malalamiko hayasikilizwi tena ndani ya chama chenye kutenda Haki nani atasikilizwa katika nchi yetu?"


Aidha, Msigwa amesema kuna watu walitegemea baada ya Matokeo ya Uchaguzi huo angetangaza kuhama chama na kujiunga na CCM lakini hana mpango huo na anayetaka jambo hilo litokee aanze kuondoka yeye..

Post a Comment

Previous Post Next Post