Mange anasema aliitwa na FBI akagoma kwenda! Yaani FBI ikuhitaji ugome au atume mtu?Haiwezani!
Dada anatupanga sana, hizi propaganda tu ili ku push deals zake.
Mange hujakatazwa kuikosoa Serikali na wala hujaombwa kumtetea Rais wetu, na wala Watanzania hawahitaji kuendelea kumchagua Rais wetu mwakani kisa vijipost vyako, bali wana kila sababu ya kuendelea kumchagua hadi 2030 kwasababu anastahili, miaka mitatu ya uongozi wake inakosha, hakuna asiyejua hili. Na wala hawezi kuongeza muda, angetaka angekubali mchakato wa katiba mpya uanze? Angesaini Sheria za Tume Huru ya Uchaguzi na Sheria ya marekebisho ya Sheria za vyama vya siaza za mwaka 2024?
Unasema tuna Rais mbaya hana alichofanya.
Ona,
Ndani ya miaka mitatu ya mhe. Rais kila sekta imekua kwa kasi isiyomithilika.
UTALII
Hii sekta imekua sana tangu Mhe. Rais Dkt Samia aingie madarakani ikichagizwa zaidi na filamu yake ya The Tanzania Royal Tour, na uimarishwaji wa mahusiano mema ya Kimataifa. Kwa Januari hadi Octoba mwaka 2023, idadi ya Watalii imeongezeka hadi kufikia 1, 471, 567 kutoka watalii 1, 175, 930 katika kipindi cha miezi hiyo mwaka 2022.
UWEKEZAJI
Kutokana na ziara tija za nje za Mhe. Rais Dkt Samia, na utekelezaji wa Sera ya uwekezaji, uwekezaji mazingira rafiki kwa Wafanyabiashara; miradi 504 yenye thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 5.6 imesajiliwa 2023 ukilinganisha na miradi 292 iliyosajiliwa 2022, hili ni ongezeko la 58%. What a wondrous news!!
KILIMO
Kwa kutambua Kilimo ndio utu wa mgongo wa Taifa letu; Serikali ya Rais Dkt Samia kwa mwaka 2023 imeongeza bajeti ya kilimo hadi kufikia bilioni 970 kutoka bajeti ya bilioni 751 ya mwaka 2022 ambalo ni ongezeko la 29% kiwango ambacho hakijawahi mithilika katika historia ya nchi yetu.
Aidha hadi kufikia Novemba 2023 Serikali imesambaza mbolea mikoa yote Tanzania bara yenye jumla ya tani 204818.16 na kutoa ruzuku ya bilioni 67.82. Unasema hana kitu?
DIPLOMASIA NA MAHUSIANO YA KIMATAIFA
Sote tunafahamu kabla ya kuingia madarakani Rais Dkt Samia, mahusiano na Mashirikiano ya nchi yetu Kimataifa yalikuwa yanachechemea; kwa mwaka 2023 Rais amefanya ziara makumi kwa makumi ndani na nje ya Bara la Afrika na hivyo kuleta mafanikio yafuatayo katika nchi:-
🌑Dola za Marekani 550 kwa ajili ya miradi ya Usalama wa Chakula
🌑 Dola la Marekani 297.64 kuwezesha mawasiliano vijijini
🌑 Chuo cha Teknolojia cha IIT Madras kutoka India kimefungua kampasi yake Zanzibar
🌑Tumepata soko la uhakika la mabondo ya samaki, parachichi, kahawa soya na kadhalika katika nchi mbalimbali duniani
🌑 Nafasi za kazi 500 kwa wauguzi wetu Saud Arabia
🌑 Tumerejeshwa kwenye mfumo wa changamoto za milenia (MCC) wa Marekani baada ya kusitishwa kwa takribani miaka 6.
🌑 Tumepokea viongozi Wakuu mashuhuri kutoka Marekani, Ujerumani, Indonesia, Hungary, Romania, pamoja na viongozi wa Nchi za Afrika.
UHURU (Kujieleza, Habari na Asasi za kiraia)
Report ya World Press Freedom ya 03/5/2024 imeonyesha Tanzania imefanya vizuri KUHESHIMU UHURU wa habari Duniani. Tumepanda toka nafasi 143 Mwaka 2023 kidunia hadi nafasi 97 Mwaka 2024. Tanzania imepanda kwa nafasi 46 na kuziacha nyuma nchi zote za Afrika ya mashariki.
Post a Comment