NMB YAKABIDHI VIFAA VYENYE THAMANI YA BILIONI 62


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameishukuru Benki ya NMB kwa kutoa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shililingi milioni 62 katika sekta za Elimu, Afya na huduma zingine za kijamii vikielekezwa kuchagiza maendeleo.

Hayo yamejili mchana wa leo Juni 06 , 2024 katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya Hospitali, Shule, kituo cha Polisi Malya na Gereza la Butimba kwenye viwanja vya Hospitali ya wilaya ya Kwimba ambapo baada ya kukabidhiwa naye amevikabidhi ili vikaanze kutumika.

Mhe. Mtanda ameongeza kuwa katika hisa za Benki hiyo asilimia 31.8 ni za Serikali lakini benki hiyo imekua bega kwa bega kusaidia wananchi kwa kushirikiana na Serikali katika mambo kadhaa wa kadhaa ya kijamii.

Aidha, amewataka wananchi wa Kwimba na wana         Mwanza wote kuichagua benki ya NMB katika huduma    za kifedha kwani wana bidhaa bora na za kisasa hususani mikopo kwa jamii katika kukuza mitaji ya biashara.

Godfrey Martine, Kaimu Meneja NMB kanda ya ziwa amesema kuwa wanajivunia kuchangia maendeleo ya wananchi kwa kutoa sehemu ya faida kwenye miradi mbalimbali hususani sekta za elimu na afya.

Aidha, amebainisha kuwa pamoja na NMB leo kutoa madawati, bati na vifaa vingine vya kuezekea, vifaa vya Hospitali, Viti na Meza kwa ajili ya kituo cha Polisi Malya, vifaa vya Magereza vikiwa na thamani ya jumla ya shilingi milioni 62 wanafanya hivyo kwa miaka saba mfululizo.


Post a Comment

Previous Post Next Post