P DIDDY AZIDI KUANDAMWA NA MABALAA HILI NI KUTOKA CHUO KIKUU..

 


Bodi ya Chuo Kikuu cha Howard, kilichojulikana kuwa "Chuo cha Watu Weusi" kilichopo Washington DC, imeazimia kumvua Sean "Diddy" Combs Shahada yake ya Heshima baada ya CNN kuonesha video ya #Diddy akimpiga mpenzi wake wa zamani Cassie hotelini

Chuo hicho kilimkabidhi Diddy Shahada hiyo Mwaka 2014 pia kimesema kimefuta Programu ya Ufadhili wa Masomo uliokuwa ukitolewa katika chuo hicho pamoja na kufuta mkataba wa Mwaka 2010 na Diddy


Makubaliano hayo yalikuwa mchango wa zaidi ya Tsh. Billion 2 ambao alitoa kupitia Taasisi yake ya Sean Combs Foundation. Taasisi hiyo haijasema chochote kuhusu hatua hiyo

Post a Comment

Previous Post Next Post