Akihojiwa na TBC1 amesema "Suala la kuondoa Umasikini ni la Nchi zote Duniani kwani hakuna Nchi iliyofanikiwa kwa Asilimia 100. Mwaka 2000 hali ya upatikanaji wa Maji Vijijini ilikuwa Asilimia 32 lakini sasa tunazungumzia Asilimia 79.8"
Aidha, upande wa Sekta ya Elimu amesema Mwaka 2000 chini ya 10% ya waliohitimu Shule ya Msingi ndio walipata fursa ya kwenda Sekondari lakini sasa kati ya Wanafunzi 100 wanaoenda Sekondari ni 70%
Juni 15, 2023, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, alisema utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Mwaka 2017/18 ulionesha 26.4% ya Watanzania walikuwa wanaishi chini ya mstari wa Umasikini wa mahitaji ya msingi kutoka 28.2% kwa Mwaka 2012.
Post a Comment