VODACOM YAFUKUZA WAFANYAKAZI NA MAWAKALA 631 KWA UDANGANYIFU...

 


AFRIKA KUSINI: Kampuni ya Huduma za Simu za Mkononi ya Vodacom imewafuta kazi Wafanyakazi na Mawakala 631 kutokana na Ripoti ya Utendaji ya Mwaka (2023/24) kuonesha ongezeko la Vitendo vya Udanganyifu wa Kimtandao katika kampuni hiyo


Ripoti ilionesha Matukio 8,652 ya Udanganyifu na Makosa mengine ya Kimtandao. Matukio 6,872 kati ya hayo ni kutoka Nje ya Kampuni na 1,780 ya Ndani ya Kampuni ambapo Watuhumiwa 15 wamekatwa 


Vodacom imesema "Kesi hizi ziliripotiwa na kutambuliwa kupitia njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Ripoti zilizopokelewa kutoka kwa Wateja, Watoa Huduma, Ripoti za Mtandaoni, Rufaa za Kibiashara, Mfumo wa usimamizi wa Udanganyifu na Watoa Taarifa wa Nje."


Post a Comment

Previous Post Next Post