GRAND FINAL YA MASHINDANO YA MISS MWANZA 2021 KUFANYIKA JULY 31.

 


Baadhi ya washiriki wa shindano la kumsaka MISS MWANZA 2021


   Shindano la kumsaka MISS MWANZA 2021 Limezinduliwa rasmi mkoani humo ili kuruhusu taratibu zingine za uendeshaji wa shindano hilo kuanza.

  Akizungumza na Mwanza Digital Mkurugenzi wa kampuni ya Universal Complex Promotions Ndg. Sebastian Kalugulu  amesema wanayo furaha kubwa kwa kupewa nafasi na kuaminiwa kuwa waandaaji wa MISS MWANZA 2021. Amesema wapo tayari kulifanya shindano hili kuwa la kipekee kwani wamefanya maboresho makubwa kutoka matamasha mengine yaliyowahi kutokea miaka kadhaa iliyopita.

 Sebastiani ameainisha baadhi ya maboresho ambayo wameyafanya kwa msimu huu ikiwa ni pamoja na zawadi itakazotoka kwa mshiriki atakaeibuka mshindi  na kuchukua taji la MISS MWANZA Ambapo mshindi atazawadiwa pesa taslimu TSH. MIL.3. Pia washiriki wote watapewa zawadi nyingi ndogo ndogo kama kifuta jasho kutokana ushiriki wao katika shindano hili.

Aidha alimaliza kwa kuwakaribisha wadau mbalimbali na wanakazi wa mkoa wa mwanza kwenye grand final ya MISS MWANZA 2021 Itakayofanyika tarehe 31 mwezi wa 7 mwaka  2021 katika jiji la Mwanza.

Post a Comment

Previous Post Next Post