Akizungumza na Mwanza Digital Mkurugenzi wa kampuni ya Universal Complex Promotions Ndg. Sebastian Kalugulu amesema wanayo furaha kubwa kwa kupewa nafasi na kuaminiwa kuwa waandaaji wa MISS MWANZA 2021. Amesema wapo tayari kulifanya shindano hili kuwa la kipekee kwani wamefanya maboresho makubwa kutoka matamasha mengine yaliyowahi kutokea miaka kadhaa iliyopita.
Sebastiani ameainisha baadhi ya maboresho ambayo wameyafanya kwa msimu huu ikiwa ni pamoja na zawadi itakazotoka kwa mshiriki atakaeibuka mshindi na kuchukua taji la MISS MWANZA Ambapo mshindi atazawadiwa pesa taslimu TSH. MIL.3. Pia washiriki wote watapewa zawadi nyingi ndogo ndogo kama kifuta jasho kutokana ushiriki wao katika shindano hili.
Aidha alimaliza kwa kuwakaribisha wadau mbalimbali na wanakazi wa mkoa wa mwanza kwenye grand final ya MISS MWANZA 2021 Itakayofanyika tarehe 31 mwezi wa 7 mwaka 2021 katika jiji la Mwanza.
إرسال تعليق