WANANCHI KATA YA KAYENZE WAGOMA KUWASUBIRI WAKANDARASI, WAUNGANA NA MBUNGE WAO KUCHIMBA MSINGI WA KITUO CHA AFYA

 Wananchi wa kata ya Kayenze wamejitokeza kwa wingi kuchimba msingi wa kituo cha Afya kinachotarajiwa kujengwa kwenye mtaa wa Nyabugali uliopo wilayani Ilemela

        Pichani ni Wananchi wa kata ya kayenze wakichimba msingi wa kituo cha                                                    afya kinachotarajiwa kujengwa hivi karibuni.


Muitikio umekuwa mkubwa baada ya serikali kupeleka Tsh. Milioni 250 kwa ajili ya kujenga kituo hicho ambacho kitapunguza changamoto ya wananchi kufuata huduma za matibabu mbalimbali huku lengo likiwa ni kumuunga mkono Rais wa Tanzania kwa kuhakikisha wanachimba msingi huo bila kusubili wakandarasi.

Hata hivyo Mbunge wa jimbo la Ilemela na Naibu waziri wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi Dr. Angeline Mabula amewataka wananchi wa kata ya Kayenze kuwa waaminifu katika mchakatato mzima wa ujenzi wa kituo hicho ambao utarajia kuanza hivi karibuni kwani kituo hicho kitasaidia kutoa huduma mbalimbali za afya.

''Tuendelee Kumuunga mkono Rais kwa kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi  ili kupunguza kero za upatikanaji wa matibabu kwa jamii, Sisi kama wasaidizi wake na ni wawakilishi wa wananchi tupo tayari kumuunga mkono ili kuhakikisha kila jambo ambalo amedhamilia kulifanya tutalisimamia katika utekelezaji wa shughuli hizo na kutambua matumizi ya pesa ili kupata kituo chenye ubora kinachokwenda na sera ya Taifa''

         Pichani ni Mbunge wa jimbo la Ilemela Dr. Angeline Mabula Akishiriki uchimbaji wa msingi wa kituo cha Afya kata ya kayenze.



Aidha Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe. Hassan Masala amewapongeza wananchi kwa kuupokea mradi  huo kwani atahakikisha fedha hizo hazikai kwenye akaunti na badala yake zitafanya kazi ambayo imekusudiwa ili kutatua changamoto kwa wananchi.
  
Mhe. Masala amemtaka mtendaji wa kata hiyo kusaidiana na kamati zilizoundwa ili kuondokana na matumizi mabaya ya fedha za mradi huo. 
    ''Tunataka kuona Fedha hizi kuanzia shilingi ya kwanza mpaka ya mwisho zionekane kwenye karatasi zimeafanya kazi gani na kila iliyookolewa na wananchi kwa kujitolea itambulike imeokolewa kiasi gani, lengo ni kupata zaidi ya haya majengo matatu kwa ukamilifu ili kumuonyesha Rais tulikuwa na shida ya kituo cha afya,  Serikali ipo pamoja na nyinyi na  itaendelea kuwa karibu na ikiwezekana kituo hiki tukikamilishe kabla ya wakati uliopangwa na kianze kutoa huduma kwani fedha tunazo, nguvu tunazo na nia tunayo na tumeanza kuzionyesha hapa''
 

             Pichani ni mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe. Hassan Masala Akishiriki uchimbaji                                                                wa msingi wa kituo cha afya kata ya kayenze

Kituo hicho kinatarajiwa kuwa na jengo la wagonjwa wa nje, maabara na eneo la kuchomea taka hivyo mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela Modest Aplinary amewataka wananchi kujitoa kwa hali na mali ili kuendelea kuokoa fedha ambazo zingetumika kulipa watu kuchimba msingi huo na ametoa matofali 10,000  yenye thamani ya  zaidi ya mil. 10 kwenye ujenzi huo.



 

Post a Comment

أحدث أقدم