AJALI DAR: WATU WAWILI WAFARIKI, NANE WAJERUHIWA

 


Watu wawili wamefariki dunia na wengine wanane kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mbezi Suka Jijini Dar es Salaam.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Muliro Jumanne Muliro amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Januari 28, 2022 ambapo watu wawili waliofariki walikuwa wakivuka kivuko cha watembea kwa miguu huku majeruhi nane wamekimbizwa hospitali iliyopo karibu na eneo hilo.

Ameongeza kuwa jeshi hilo linamsaka dereva aliyesababisha ajali hiyo ambaye alikimbia.

"Kwenye zile tafrani dereva alishuka na kukimbia lakini tunauhakika hana uwezo wa kufika mbali, atakamatwa na hatua za kisheria dhidi yake zitachukuliwa"-Kamanda Muliro.

Endelea kufutilia Mwanza Digital Habari kwa Taarifa zaidi.

Post a Comment

أحدث أقدم