WAGOMBEA 9 WA USPIKA WA BUNGE WATAKAOPIGIWA KURA KESHO FEBRUARI MOSI 2022




Katibu wa Bunge  na msimamizi wa uchaguzi wa Spika Nenelwa Mwihambi(NDC) , amesema hadi kufikia leo saa Kumi Jioni Majina ya jumla ya Wagombea Tisa (9) yalikuwa yamewasilishwa na kukidhi matakwa ya kisheria kwa ajili ya uchaguzi wa Spika unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 1 Februari, 2022.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma, Katibu wa Bunge amesema kuwa miongoni mwa Wagombea hao nane sio Wabunge na mmoja ni Mbunge.


Amewataja wagombea hao kuwa ni Abdullah Mohammed Said (NRA), Mhandisi Aivan Jackson Maganza (TLP), David Daud Mwaijojele (CCK), Georges Gabriel Bussungu (ADA -TEA), Kunje Ngombale Mwiru (SAU),

Wengine Maimuna Said Kassim (ADC), Ndonge Said Ndonge (AAFP), Saidoun Abrahamani Khatib (DP) na Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson.

NDC mwihambi Ametumia fursa hiyo kuwashukuru wagombea wa vyama vyote vya siasa waliojitokeza katika zoezi hilo huku akiwataka kufika mapema Bungeni hapo kesho ambapo atawasilisha majina yao mbele ya wapiga kura ambao ni waheshimiwa wabunge.
Mwisho

Post a Comment

أحدث أقدم