MAFURIKO YAUA WATU TISA AKIWEMO MTOTO


Takribani watu tisa, akiwemo mtoto mmoja wamefariki kufuatia mafuriko ya mvua kubwa na maporomoko ya udongo yaliyotokea katika wilaya ya Kisoro kusini-magharibi mwa  nchi ya Uganda.

Shrika la msalaba mwekundu la Uganda limethibitisha kutokea kwa janga hilo usiku wa kuamkia jana januari 25,2022 ambapo katika marehemu hao miili nane imefukuliwa jana asubuhi.

"Wa tisa ni mtoto ambaye aliangukiwa na udongo wakati alipokuwa akikimbia. Kwahiyo hakuna anayejua ni wapi hasa pa kuchimba ,"lilisema.

Mvua kubwa imeharibu nyumba, barabara, na miundo mbinu.

Leo shirika hilo la msaada mwekundu Nchini Uganda limetoa msaada wa dharura kwa familia 300 zilizoathiriwa na janga la mvua kubwa na mafuriko huko Kisoro.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI 







Post a Comment

أحدث أقدم